Nenda kwa yaliyomo

Iota

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Alfabeti ya Kigiriki
Herufi za kawaida
Α α Alfa 1 Ν ν Ni 50
Β β Beta 2 Ξ ξ Ksi 60
Γ γ Gamma 3 Ο ο Omikron 70
Δ δ Delta 4 Π π Pai 80
Ε ε Epsilon 5 Ρ ρ Rho 100
Ζ ζ Dzeta 7 Σ σ ς Sigma 200
Η η Eta 8 Τ τ Tau 300
Θ θ Theta 9 Υ υ Ipsilon 400
Ι ι Iota 10 Φ φ Phi 500
Κ κ Kappa 20 Χ χ Khi 600
Λλ Lambda 30 Ψ ψ Psi 700
Μ μ Mi 40 Ω ω Omega 800
Herufi za kihistoria1
Digamma 6 San 90
Stigma 6 Koppa 90
Heta 8 Sampi 900
Yot 10 Sho 900
1 Viungo vya nje:
Alfabeti_ya_Kigiriki#Viungo_vya_nje

Iota (pia: yodi) ni herufi ya tisa katika Alfabeti ya Kigiriki. Umbo la iota kubwa na ndogo limeendelea vilevile katika alfabeti ya Kilatini na hivyo hutumiwa vile hadi leo katika lugha zote zinazotumia mwandiko huo kama vile Kiswahili, Kiingereza na kadhalika.

Kwa matumizi ya tarakimu inamaanisha namba 10.[1]

Matamshi yake ni sawa na "i" kwa Kiswahili.

Neno iota = yodi katika tafsiri ya Biblia

[hariri | hariri chanzo]

Katika tafsiri ya Biblia ya "Union Bible" neno "yodi" hutumiwa pale ambako lugha asilia ya Kigiriki inatumia "iota" .

Math 5:18: Kwa maana, amin, nawaambia, mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya Torati haitaondoka, hata yote yatimie. [2]

Hapa neno iota/yodi hutumiwa kumaanisha "herufi ndogo kabisa" yaani sehemu ndogo yoyote ya Maandiko matakatifu.

  1. Iota ina maana ya kumi ingawa ni herufi ya tisa. Sababu yake ni kwamba alama ya digamma imepotea katika alfabeti lakini imebaki kama tarakimu ya "sita"
  2. Mathayo 5:18 kwenye intaneti