Belarus
| |||||
Kaulimbiu ya taifa: -- | |||||
Wimbo wa taifa: Belarusian: Мы, беларусы (Mi Belarusi) ("Sisi Wabelarus") | |||||
Mji mkuu | Minsk | ||||
Mji mkubwa nchini | Minsk | ||||
Lugha rasmi | Kibelarus, Kirusi | ||||
Serikali | Jamhuri Alexander Lukashenko Roman Golovchenko | ||||
Uhuru Ilitangazwa ilianzishwa ilikamilishwa |
27 Julai 1990 25 Agosti 1991 25 Desemba 1991 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
207,600 km² (ya 84) kidogo sana (183 km²)[1] | ||||
Idadi ya watu - 2016 kadirio - 2009 sensa - Msongamano wa watu |
9,498,700 (ya 93) 9,503,807 45.8/km² (ya 142) | ||||
Fedha | Rubel ya Belarus (BYN )
| ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
FET (UTC+3) FET (UTC+3) | ||||
Intaneti TLD | .by | ||||
Kodi ya simu | +375
- |
Belarus (kwa Kibelarus: Беларусь (Kikyrili) au Biełaruś (Kilatini); kwa Kirusi:Белоруссия ) ni nchi ya Ulaya ya Mashariki inayopakana na Urusi, Ukraine, Poland, Lithuania na Latvia.
Mji mkuu ni Minsk na miji mingine ni pamoja na Brest, Grodno, Gomel, Mogilev na Vitebsk.
Idadi ya wakazi inapungua: ni watu 9,498,700 (2016).
Historia
[hariri | hariri chanzo]Belarus haikuwahi kuwa nchi ya pekee hadi karne ya 20. Maeneo yake yalikuwa chini ya himaya mbalimbali kama vile Poland, Lithuania na Urusi. Belarus ilikuwa kitengo cha Umoja wa Kisovyet tangu 1919/1922 hadi 1991.
Wakazi na utamaduni
[hariri | hariri chanzo]Wakazi walio wengi ni Wabelarus (83.7%) ambao wanaongea ama Kibelarus au Kirusi ambavyo vyote viwili ni lugha rasmi. Lugha hizi mbili zina asili moja. Takriban 11% za wakazi ni Warusi.
Kuna pia vikundi vidogo vinavyotumia lugha za pekee kama vile Kipoland, Kiukraine, Kilatvia, Kilituanya na nyingine.
Walio wengi ni wafuasi wa Ukristo katika Makanisa ya Kiorthodoksi (48.3%) na katika Kanisa Katoliki (7.1%).
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- Tovuti rasmi ya mji wa Minsk Archived 2 Novemba 2017 at the Wayback Machine.
Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Belarus kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |