The Proposal
The Proposal | |
---|---|
Imeongozwa na | Anne Fletcher |
Imetayarishwa na | Todd Lieberman David Hoberman Alex Kurtzman Roberto Orci Kristin Burr |
Imetungwa na | Peter Chiarelli |
Nyota | Sandra Bullock, Ryan Reynolds, Malin Akerman Mary Steenburgen Craig T. Nelson Betty White Oscar Nuñez Aasif Mandvi |
Muziki na | Aaron Zigman |
Imehaririwa na | Amanda Mackey Johnson Cathy Sandrich |
Imesambazwa na | Touchstone Pictures |
Imetolewa tar. | Juni 1, 2009 |
Ina muda wa dk. | Dakika 108 |
Nchi | Marekani |
Lugha | Kiingereza |
Bajeti ya filamu | $40 million[1] |
Mapato yote ya filamu | $314,658,031[1] |
The Proposal ni filamu ya kuchekesha iliyotolewa 2009, iliyoongozwa na Anne Fletcher na kuigizwa na Sandra Bullock na Ryan Reynolds. Filamu hii ilitungwa na Pete Chiarelli.[2]
Hadithi
[hariri | hariri chanzo]Margaret Tate ni mhariri mkuu wa kampuni ya kuchapisha vitabu inayoitwa Ruick & Hunt Publishing. Wafanyikazi wake hawapendi uongozi wake. Baada ya kupata habari kuwa atarudishwa kwao nchini Canada, yeye anamlazimisha mtumishi wake, Andrew Paxton, amuowe ili apate kubaki nchini Marekani. Andrew anakubali kumuoa Margaret, lakini kwa masharti.
Wawili hawa wanaenda likizo kwa wazazi wa Andrew, kijijini Sitka, Alaska ili kuwadangaya familia yao kuwa wanaowana. Margaret anashikwa na bumbuwazi pindi anapogundua kuwa familia ya kina Andrew ni matajiri wanaomiliki biashara nyingi kijijini Sitka. Baada ya sherehe iliyoandaliwa nyumbani, Andrew anatangaza kuwa atamuowa Margaret.
Familia ya Andrew ilipokea habari hizo kwa furaha (isipokuwa babake Andrew) na wanapanga kuwa harusi ifanywe wiki hiyo hiyo. Harusi inapofanyika Margaret anaamua kuwa hawezi kuolewa na Andrew, na anatubia mbele ya kila mtu kuwa hiyo ilikuwa harusi ya uwongo. Margaret anaarifiwa kuwa ana saa 24 za kurudi Canada. Kwa sababu Margaret alikubali hatia aliyofanya, Andrew hakupelekwa jela. Margaret alirudi New York, na kufunganya vitu vyake. Andrew anakimbilia kumfuata na anampata Margaret ofisini anapomuambia kuwa anampenda mbele ya watu wote ofisini. Andrew anamposa Margaret, na wawili hawa na wachumba, na mara hii ni "kikwelikweli".
Waigizaji
[hariri | hariri chanzo]- Sandra Bullock aliigiza kama Margaret Tate, mhariri mkuu wa kampuni ya kuchapisha vitabu.
- Ryan Reynolds aliigiza kama Andrew Paxton, anayekubali kumuoa Margaret kwa sharti la kupandishwa cheo cha mhariri.
- Mary Steenburgen anayeigiza kama Grace Paxton, mamake Andrew.
- Craig T. Nelson aliigiza kama Joe Paxton, babake Andrew anayemtaka Andrew amiliki biashara alizonazo kijijini Sitka.
- Betty White aliigiza kama Annie, nyanyake Andrew.
Kurekodi filamu
[hariri | hariri chanzo]Ingawa filamu hii ilichukuliwa kijijini Sitka, filamu hii ilirekodiwa katika eneo la Cape Ann mjini Massachusetts.
Muziki
[hariri | hariri chanzo]Ilitungwa na Aaron Zigman aliyerekodi nyimbo zake kwenye studio ya Hollywood Studio Symphony.[3]
Mafanikio
[hariri | hariri chanzo]Kwenye siku yake ya kwanza, filamu hii iliuza tikiti za milioni $12.7 kutoka kwa sinema 3,056, na kuwa namba 1 siku hiyo..[1][4] Filamu hii ilipata milioni $314 kote duniani na kuifanya filamu mojawapo ya Sandra Bullock iliyopata mafanikio iliyokusanya $163,958,031 kutoka nchi ya Marekani na Canada.
DVD
[hariri | hariri chanzo]The Proposal ilitolewa kwa DVD mnamo 13 Oktoba 2009.[5] Baada ya wiki mbili, iliuza nakala za DVD 3,314,840 na kupata $54,744,965.[6]
Tuzo
[hariri | hariri chanzo]Sandra Bullock alichaguliwa kwa tuzo la Golden Globe Award na akashinda tuzo la Teen Choice Award..[7] Pia, alishinda tuzo la People's Choice Award kwa kuwa muigizaji bora.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ 1.0 1.1 1.2 "The Proposal (2009)". Box Office Mojo. Iliwekwa mnamo 2009-06-22.
- ↑ The Proposal (2009)
- ↑ Dan Goldwasser. "Aaron Zigman scores The Proposal", ScoringSessions.com, 2009-05-06. Retrieved on 2009-05-06.
- ↑ [1]
- ↑ Thorton, Michelle (17 Agosti 2009). ""The Proposal" On DVD October 13th". ReelEmpire.com. Iliwekwa mnamo 18 Agosti 2009.
- ↑ [2] Archived 8 Novemba 2009 at the Wayback Machine..
- ↑ https://www.eonline.com/uberblog/b158058_complete_list_of_2010_golden_globe.html
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Tovuti rasmi ya The Proposal
- The Proposal at the Internet Movie Database
- (Kiingereza) The Proposal katika Allmovie
- The Proposal katika Metacritic
- The Proposal katika Sanduku la Ofisi la Mojo
- The Proposal at Rotten Tomatoes