Nenda kwa yaliyomo

Scandal (mfululizo wa filamu)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Filamu hii inaangazia maisha yaliyojaa misukosuko ya Olivia Pope

Scandal ni kipindi cha televisheni kinachorushwa kama filamu ya kusisimua na ya kisiasa kutoka nchini Marekani. Filamu hii inaigizwa na mwigazi maarufu Kerry Washington na kuandaliwa na Shonda Rhimes. Ilionyeshwa kwenye shirika la ABC kuanzia Aprili 5, 2012, hadi Aprili 19, 2018, kwenye vipindi 124 katika misimu saba (seasons). [1]

Wasifu wa muigizaji Kerry Washington, Olivia Pope, katika filamu hii umeegemezwa sehemu kubwa kama vile ilivyokuwa kwa msaidizi wa zamani wa utawala wa George H. Bush Judy Smith, ambaye pia anahudumu kama mtayarishaji mwenza. [2]

Filamu hii kubwa ya kusisimua inachukua hadhira ya mji mkuu wa Marekani Washington, D.C. na kuangalizia sana kampuni ya Olivia Pope ya kudhibiti na kutoa huduma ya utatuzi wa matatizo mbalimbali ya kijamii hususani ya kisheria , Olivia Pope & Associates (OPA), na wafanyakazi wake, pamoja na wafanyakazi katika Ikulu ya White House na eneo la kisiasa linalozunguka ikulu hiyo ya Marekani. Mbali na Kerry Washington, kipindi hicho kinamshirikisha Tony Goldwyn kama Fitzgerald Grant III, Rais wa Marekani—baadaye Raisi wa zamani—na Mpenzi wa Olivia; Darby Stanchfield kama Abby Whelan, msaidizi katika OPA (baadaye iliitwa Quinn Perkins & Associates au QPA), na pia aliyekuwa Katibu wa Vyombo vya Habari wa Ikulu ya White House na Mkuu wa Wafanyakazi; Katie Lowes kama Quinn Perkins, msaidizi wa zamani katika OPA na baadaye mkuu wa QPA; Guillermo Diaz kama Huck, wakala wa zamani wa shirika la kijasusi liitwalo B613 na msaidizi katika QPA; Jeff Perry kama Cyrus Beene, Mkuu wa zamani wa Ikulu ya White House chini ya Grant na baadaye Makamu wa Rais wa Marekani chini ya Mellie Grant; Joshua Malina kama David Rosen, Mwanasheria Mkuu wa Serikali; Bellamy Young kama Mellie Grant, mke raisi wa zamani, seneta wa zamani, na baadaye Rais wa Marekani baada ya Grant; Scott Foley kama Jake Ballard, Mkurugenzi wa NSA na mpenzi wa pili wa Olivia; Cornelius Smith Jr. kama Marcus Walker, mwanaharakati wa haki za kiraia, ambaye aliwahi kuwa msaidizi wa OPA na Katibu wa Vyombo vya Habari vya Ikulu ya White House; Joe Morton kama Eli "Rowan" Papa, baba yake Olivia na mkuu wa zamani wa B613; na George Newbern kama Charlie, wakala wa zamani wa B613 ambaye baadaye anakuwa mwanachama wa QPA.

Kipindi hicho cha filamu kilikuwa Kipindi Bora cha Televisheni cha Mwaka na Taasisi ya Filamu ya Marekani, kilipokea Tuzo ya Peabody kwa Ubora katika Televisheni na kilitunukiwa sifa ya Filamu bora katika Tuzo za Picha. Washington alishinda Tuzo ya Picha ya Mwigizaji Bora katika Mfululizo wa filamu hii na teuliwa kwenye Tuzo za Emmy kama Mwigizaji Bora wa Kina katika Mfululizo wa filamu hii, pia Tuzo ya Golden Globe ya Mwigizaji Bora na Tuzo ya SAG . Kipindi hicho pia kiliweka historia wakati Kerry Washington alipoigizwa kama Olivia Pope, akawa mwanamke wa kwanza Mwafrika kuigiza tamthilia ya Kimarekani kwenye televisheni inayofuatiliwa na watu wengi marekani katika karibu miaka arobaini.

Msimu wa 1

[hariri | hariri chanzo]

Msimu wa kwanza wa Scandal ilimtambulisha Olivia Pope (Kerry Washington) na wanachama mbalimbali katika kampuni yake. Aidha, ilimtambulisha Rais wa Marekani, Fitzgerald Grant III (Tony Goldwyn) na mkuu wake wa wafanyakazi Cyrus Beene ( Jeff Perry ). Msimu huu unaangazia maisha ya washiriki, uhusiano kati ya Olivia na Rais (mwajiri wake wa zamani), na siri inayozunguka ushiriki wa Amanda Tanner (Liza Weil) na Ikulu ya White House, kati ya kesi zingine ambazo timu ilikuwa imetatua.

Msimu wa 2

[hariri | hariri chanzo]

Jaribio la mauaji linafanywa kwenye maisha ya Fitz, ambayo karibu kuuwawa. Matokeo yake, Sally Langston ( Kate Burton ) anachukua nafasi ya rais, kiasi cha kusikitishwa na kukerwa na Cyrus ambaye hakupenda uamuzi huo kwakuwa hali ya raisi huwenda isingepelekea kupoteza maisha. Baada ya kunusurika, Fitz anaamua kumpatia talaka mke wake, ambapo kewe Mellie ( Bellamy Young ) anajaribu kumshawishi daktari wake wa uzazi kumpa muda akiwa leba ili asipate talaka hio. Huck ( Guillermo Díaz ) anakamatwa kwa jaribio la mauaji baada ya kuingizwa katika mtego na mpenzi wake Becky (Susan Pourfar). Baada ya David ( Joshua Malina ) kumsaidia Huck kwenda huru, Huck, Olivia na timu yake kumlaghai Becky ili ajitokeze katika hospitali ambako amekamatwa. Fitz anagundua kuwa Verna ( Debra Mooney ) alikuwa nyuma ya mauaji hayo na anamuua. Katika mazishi, anafichua kwa Olivia kwamba hataki talaka kwani amevunjika moyo baada ya kujua juu ya wizi kutoka kwa Verna ambaye alikuwa ni rafiki yake wa karibu na ambaye alimsaidia sana katika kupata uraisi wake.

Msimu huu unaangazia kumtafuta msaliti ambaye anavujisha habari za siri kutoka Ikulu ya Marekani. Olivia na timu wanachunguza kesi hiyo baada ya kubaini kuwa kujiua kwa Mkurugenzi wa CIA ni mauaji na yalitendeka kwa kumtishia mkurugenzi huyo hadi kujiuwa. Olivia anapata kujuana na Kapteni Jake Ballard ( Scott Foley ), ambaye anafanya kazi na kiongozi wa B613, Rowan ( Joe Morton ), ambaye anaamuru Jake kuwa karibu na Olivia. Mwishoni mwa msimu, Mellie anampa Fitz hati ya mwisho na kwamba atakuwa mwaminifu, na anaenda kwenye runinga ya kitaifa na kufichua uchumba wa Fitz na Olivia. Fitz anamchagua Olivia, jambo ambalo linamfanya Mellie afichue jambo hilo. Fitz atangaza kampeni yake ya kuchaguliwa tena. Wakati Olivia na timu wanaendelea kuchunguza msaliti ni nani, Huck anafanikiwa kumkamata Charlie ( George Newbern ), ambaye anafichua utambulisho wa kama msaliti: Billy Chambers ( Matt Letscher ),Waligundua kuwa Billy anafanya kazi na David, ambaye anaiba kadi ya Cytron, lakini anamtengenezea Billy na kumpa Cyrus kadi hiyo ili kurejeshwa kama Mwanasheria wa Marekani. Mwishowe, jina la Olivia linavuja kwa waandishi wa habari kama mchepuko wa raisi Fitz, na inafichuliwa kuwa Rowan ndiye baba yake Olivia.

Msimu wa 3

[hariri | hariri chanzo]

Baada ya jina la Olivia kujulikana na waandishi wa habari kuwa ndiye mwanamke mchepuko wa Raisi fitz kampuni ya Olivia Pope & Associates ikapitia kipindi kigumu kupata kazi kutoka kwa wateja wao na hivyo kupitia hali mbaya kifedha.

Kampuni inaanza kuchukuwa wateja wapya kabisa tofauti na wale wa zamani ilikuweza kulipia kodi. Rowan anazidi kuingia na kujihusisha na maisha ya Olivia,ambacho kitendo hicho kinaleta madhara kwenye maisha ya Olovia,na kupelekea Huck na Jake kuanza upelelezi wa shirika la siri la B613.Waligundua kuwa katika tukio la kijeshi lilioitwa “Operesheni Remington”,Fitz aliidungua ndege ya abiria huko Iceland huku mama yake Olivia akiwa ni mmoja wapo wa wahanga 300 katika tukio hilo. Kuzidi kufatila ukweli wa tukio hilo,walikuja kugundua kuwa mmoja ya abiria aliyetakiwa kupanda ndege hio alishushwa kabla ya ndege hio kuondoka. Quinn (Katie Lowes) akaanza kuzidi kuwa karibu na Charlie,mpaka kuanguka katika mtego wa kumuuwa mlinzi mmoja ambaye ndiye alikuwa ahusike katika ushahidi wa abiria gani aliye shushwa katika ndege ile kabla ya kuondoka. Kutokana na tukio hilo alilolifanya Quinn la mauaji Huck anamteka na kumtesa na hivyo kuondoka katika kampuni yao.

Huku Fitz akikumbana na tatizo kutoka kwa kiongozi Josephine "Josie" Marcus (Lisa Kudrow) amabaye amechukua nafasi ya kugombea akikinzana na Seneta Samuel Reston (Tom Amandes) akitumia mgongo wa chama cha demokrati huku kuwania nafasi ya Raisi wa marekani na kuwa raisi wa kwanza wa kike kuwahi kutokea. Cyrus akijaribu kadiri ya uwezo wake kutafuta machafu ya Marcus ilikuharibu kampeni zake,lakini alishindwa. Baada ya Olivia kutambua kuwa Fitz alihusika katika tukio la kuishambulia ndege ya abiria,ameamua kujitoa kuwa kama kampeni meneja katika kampeni zake za uraisi na kuamua kuwa meneja wa Josephine Marcus'

  1. Seidman, Robert (Mei 17, 2011). "ABC 2011–12 Primetime Schedule Announced". TV by the Numbers. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Machi 26, 2016. Iliwekwa mnamo Januari 10, 2012.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. Tucker, Neely. "ABC bases 'Scandal' on D.C. insider Judy Smith", The Washington Post, March 30, 2012.