Nenda kwa yaliyomo

Namba za simu Tanzania

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Namba za simu nchini Tanzania zinatolewa chini ya kanuni za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (Tanzania Communication Regulatory Authority - TCRA).

Mamlaka hii inatoa laiseni kwa ajili ya makampuni ya huduma za mawasiliano pamoja na simu na intaneti. Kanuni zake zinatawala fomati za namba za simu.

Fomati za namba

Simu ya waya (ya kawaida) ndani ya mtandao wa kieneo hupigwa kwa namba yake pekee. Kama iko katika eneo tofauti ni lazima kutangulia namba ya eneo, mfano kwa Dar es Salaam 022 au kwa Dodoma 026. Mfano simu namba 667788 ya Dar es Salaam inafikiwa kutoka mikoani kwa 022 667788.

Simu za mkononi hupatikana kila wakati kupitia namba za mitandao ya makampuni kwa namba kama 0624112233.

Kupiga namba nje ya nchi inahitaji namba ya kimataifa. Namba za kimataifa hutanguliwa kwa 00 au alama ya +. Ile sifuri ya namba ya eneo inaachwa hapa. Kupiga namba ya Tanzania kutoka nje inatanguliwa kwa 00255 inayofuatwa na namba ya eneo au mtandao bila sifuri.

  • Kupiga namba ya kawaida ya juu kutoka ng'ambo ni +255 (sawa na 00255) 22 667788.
  • Kupiga namba ya juu kutoka ng'ambo ni lazima kutumia +255 (sawa na 00255) 624 11 22 33.

Namba za kieneo katika Tanzania

Kwa mawasiliano ndani ya Tanzania namba za kieneo hutanguliwa na "0". Kufikia simu kutoka nje ya nchi kuna namba ya kimataifa 00255 (sawa na +255) inayofuatiliwa na namba ya kieneo bila 0 na namba ya simu.

Namba za kieneo[1]
22 Dar es Salaam
23 Pwani, Kibaha, Kisarawe, Lindi, Morogoro, Mtwara
24 Zanzibar (Unguja & Pemba, pamoja na Chake Chake, Mkoani, Wete)
25 Mbeya, Rukwa, Ruvuma
26 Dodoma, Iringa, Nzega, Singida, Tabora
27 Arusha; Kilimanjaro, Moshi, Tanga
28 Bukoba, Kagera, Kigoma, Mara, Mwanza, Shinyanga

Namba za simu za mkononi

Namba hizi huanza kwa 6 au 7 na kuwa na tarakimu 9 (bila sifuri).

Simu za mkononi Tanzania[2]
Namba ya mtandao Kampuni
62 Halotel (Viettel)
65 TIGO (Mobitel)
66 Smile Communications Tanzania Limited
67 TIGO (Mobitel)
68 Airtel Tanzania Limited
69 Airtel Tanzania Limited
71 TIGO (Mobitel)
73 TTCL Tanzania Telecommunications Company Ltd
74 Vodacom (Celtel)
75 Vodacom (Celtel)
76 Vodacom (Celtel)
77 Zantel (Zanzibar Telecom Ltd)
78 ZAIN

Historia

Tanzania, Kenya na Uganda zilirithi mtandao wa simu wa pamoja kutoka enzi za ukoloni. Kwa hiyo mawasiliano kati ya Dar es Salaam na Nairobi au Kampala hazikuwa simu za kimataifa. Kulikuwa na mfumo na namba za kieneo kwa Afrika ya Mashariki yote iliyotawaliwa na huduma ya posta ya pamoja iliyoitwa East African Posts and Telecommunications Administration. Mtandao huu wa pamoja uliendelea hata baada ya kuporomoka kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki lakini baadaye shirika za posta zilianza na mipango ya pekee katika kila nchi. Tanzania ilitoka katika mfumo wa pamoja mwaka 1999. Lakini hadi sasa si lazima kutumia namba ya kimataifa inatosha kutumia namba za pekee za kikanda: kupiga simu Kenya ni 005 badala ya 00254, kupiga simu Uganda ni 006 badala ya 00256. Tanzania inafikiwa kwa 007 si lazima kutumia 00255.

Tanbihi

  1. https://www.itu.int/oth/T02020000CB/en
  2. https://www.itu.int/oth/T02020000CB/en