Kofia
Mandhari
Kofia ni vazi la kichwani lenye umbo la kikapu na ukubwa unaomfaa mhusika.
Aina za kofia maarufu Afrika Mashariki
[hariri | hariri chanzo]- Kofia ya baraghashia: ni ya vitambaa na ina vitundu vingi vinavyodariziwa kwa kufumwa na uzi wa rangi ya fedha. Jina lake linatokana na jina la sultani Barghash bin Said wa Zanzibar aliyeliingiza Unguja kwa mara ya kwanza.
- Kofia ya chepeo ina upeto unaofunika sehemu ya mbele
- Kofia ya kazi / kofia ya bulibuli ni nyeupe na imedariziwa
- Kofia ya pama ina ukingo mpana unaozunguka pande zote kama kinga dhidi ya ukali wa jua
- Kofia ya topi haina chepeo na kwa kawaida huvaliwa na wanawake
- Kofia ya tunga / tarabushi ni ya duara, ya rangi nyekundu na ina tarabushi upande wa nyuma
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kofia kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |