Nenda kwa yaliyomo

Kobe (kundinyota)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nyota za Kobe (Corona australis) katika sehemu yao angani
Ramani ya kundinyota la Kobe (Corona Australis) jinsi inavyoonekana kwa mtazamaji kwenye nusutufe ya kaskazini ya Dunia
Nyota za kundinyota la Kobe (Corona Australis) jinsi zilivyochorwa miaka 200 iliyopita pale Ulaya

Kobe (Corona Australis kwa Kilatini na Kiingereza) [1] ni jina la kundinyota kwenye angakusi ya Dunia.

Mahali pake

Kobe ni kundinyota dogo linapakana na Mshale (pia Kausi au lat. Sagittarius) upande wa kaskazini na Nge (pia Akarabu, lat. Scorpio) upande wa magharibi, , Darubini (Telescopium) upande wa kusini, na Madhabahu (Ara) upande wa kusini magharibi.

Jina

Kobe lilijulikana kwa jina hili kwa miaka mingi kati ya mabaharia Waswahili waliotumia nyota kutafuta njia baharini wakati wa usiku.[2] Jina la Kobe lilipokelewa na Waarabu walioijua zamani kwa jina la قبه qubba kutokana na umbo lake maana nyota hukaa kama nusuduara[3]. Umbo hili linaweza kufafanishwa na umbo la mnyama kobe.

Wagiriki wa Kale waliona hapa shada la heshima la majani jinsi walivyowapa washindi wa michezo. Shada la heshima liliendelea baadaye kutazamiwa kama taji na hapo asili ya jina la kimataifa “Corona” linalomaanisha taji. Ilhali kuna kundinyota mbili zinazoitwa Corona zinatofautishwa kwa kuitwa ya kaskazini na ya kusini, hivyo Kobe ni Corona Australis (zamani pia Corona Austrina, kwa maana hiyohiyo).

Kobe ni kati ya makundinyota yiliyotajwa tayari na Klaudio Ptolemaio katika karne ya 2 BK kwa jina la Στεφανος νοτιος stefanos notios (Shada la Kusini).[4] Iko pia katika orodha ya makundinyota 88 ya Umoja wa Kimataifa wa Astronomia [5] kwa jina la Corona Australis. Kifupi chake rasmi kufuatana na Ukia ni 'CrA­'.[6]

Nyota

Kobe ina nyota 21 zinazoweza kuangaliwa kwa macho matupu lakini hazingai sana.

Jina la
(Bayer)
Namba ya
Flamsteed
Jina
(Ukia)
Mwangaza
unaoonekana
Umbali
(miakanuru)
Aina ya spektra
β 4,10m 400 G7 II
α Meridiana[7] 4,1m 100 A2 V
γ 4,23m 120 F8 + F8
δ 4,57m 200 K1 III

Tanbihi

  1. Uhusika milikishi (en:genitive) ya neno "Corona Australis" katika lugha ya Kilatini ni "Coronae Australis" na hili ni umbo la jina linaloonekana katika majina ya nyota za kundi hili kama vile Alfa Coronae Australis, nk.
  2. ling. Knappert 1993
  3. Lane, Arabic-English lexicon (1872), vol. 7, uk. 2488
  4. Allen, Star-names, uk. 172
  5. The Constellations, tovuti ya International Astronomical Union , iliangaliwa Julai 2017
  6. Russell, Henry Norris (1922). "The New International Symbols for the Constellations". Popular Astronomy. 30: 469–71. Bibcode:1922PA.....30..469R.
  7. ling. tovuti ya Ukia: Naming stars


Marejeo

  • Richard Hinckley Allen: Star-Names and their Meanings; kwa G. E. Stechert New York, Leipzig, London, Paris 1899, ukurasa 75 ff (online hapa kwenye archive.org)
  • Jan Knappert, 1993: The Swahili Names of Stars, Planets and Constellations; The Indian Ocean Review September 1993 Volume 6 No. 3 September 1993, kurasa 6-7, ISSN 1031-2331
  • Lane, Edward William : An Arabic - English Lexicon by in eight parts – 1872 (Perseus Collection Arabic Materials Digitized Text Version v1.1 of reprint Beirut – Lebanon 1968) online hapa
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kobe (kundinyota) kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.