Kizio
Kizio ni kiasi cha upimaji ambacho kimekubaliwa kutumika kama kipimo sanifu. Jumla la vitu hugawiwa kwa vizio vilevile kwa kusudi ya kulinganisha jumla hii na kiasi kingine cha kiti kilekile.
Kwa mfano urefu unaweza kupimwa kwa njia mbalimbali. Kulinganisha uzito wa bidhaa kunahitaji vizio vilivykubaliwa.
Zamani watu walikuwa na vizio vya upimaji tofauti kila mahali.
Vipimo sanifu vya kimataifa
[hariri | hariri chanzo]Tangu karne ya 19 kuna utaratibu wa vipimo sanifu vya kimataifa (SI) na vizio vyao ni vilevile kote duniani.
- Vizio vya upimaji wa urefu ni mita, kilomita au sentimita.
- Vizio vya upimaji vya uzani ni gramu, kilogramu na tani.
- Vizio vya upimaji vya mjao ni lita, mililita.
- kuna vizio vingine kwa kila tabia inayohitaji kupimwa.
Vizio vingine
[hariri | hariri chanzo]Vipimo vya SI vimekubaliwa zaidi na zaidi lakini si vyote katika kila nchii kwa sababu kuna bado desturi za kitaifa zinazopendelea vizio wanavyozoea tangu kale.
Nchi zilizoathiriwa na Uingereza pamoja na Marekani huendelea kutumia vizio vya vipimo va Uingereza kama futi, inchi na maili kwa urefu, galoni kwa mjao au pauni (ratili) kwa uzani. Vizio hivi vinaendelea kutumiwa na watu hata kama rasmi nchi nyingi zimeshakubali vipimo vya SI.
Kwa jumla vipimo vya Uingereza pamoja na nchi nyingi za Ulaya viliendeleza utaratibu wa vizio vya vipimo vya Kiroma kwa kuchanganya na desturi za kikabila.
Vipimo hivi vya kale vilitegemea mara nyingi ukubwa wa mguu, mkono, urefu wa hatua kwa sababu hivi vilikuwa vipimo vilivyofanana kati ya watu. Isipokuwa baada ya kusanifisha vipimo asilia hivi ilionekana ya kwamba vilikuwa tofauti kati ya eneo na eneo au nchi na nchi. Kwa mfano katika Ujerumani palikuwa na vizio vya futi makumi kati ya urefu wa sentimita 25 hadi sentimita 33.5.
Tofauti hizi pamoja na mahitaji ya biashara yalisababisha kuundwa kwa utaratibu mpya wa vipimo sanifu kwanza vya kitaifa na baadaye vya kimataifa.
Pamoja na vipimo vya kale kuna aina moja ya pekee ya vizio visivyolingana na utaratibu wa SI na hivi ni vipimo vya astronomia. Kwa kusudi la kuepukana na namba kubwa mno zinazotokea kama vipimo kama kilomita vinatumiwa kwa umbali katika anga la ulumwengu wataalamu wa astronomia walipatana kutumia vipimo kama mwakanuru, kizio astronomia na parsek visivyolingana na muundo wa SI.