Kigweno
Kigweno (pia huitwa Kighonu) ni lugha ya Kibantu nchini Tanzania inayozungumzwa na Wagweno. Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kigweno iko katika kundi la E60. Lugha ya Kigweno huingiliana na lugha ya Kikamba na lugha ya Kichaga kwa kiasi fulani.
Mwaka wa 2006 idadi ya wasemaji wa Kigweno imehesabiwa kuwa watu 2200. Lugha inazungumzwa katika Wilaya ya Mwanga hasa katika maeneo ya Kifula, Kikweni, Lambo, Mangio, Masumbeni, Mcheni, Msangeni, Mwaniko, Simbomu, Vuchamana maeneo ya Shighatini kwa kiwango kidogo. Kutokana na uenezaji huu kuna dalili ya kuwa wazungumzaji wa Kigweno ni wengi kuliko ilivyoelezwa katika marejeo ya kitaalamu yaliyotajwa hapo juu. Tarafa yote ya Ugweno huzungumza Kigweno kama Lugha mama na Kiswahili ni lugha ya pili.
Wagweno wakati mwingine huweza kuwa mahiri wa kuzungumza lugha ya Kipare ambapo Wapare wao hawajui Kigweno wao hubakia na lugha moja tu ya Kipare ambacho huzungumzwa Usangi na maeneo ya Mwanga yaani tambarare na maeneo ya Wilaya ya Same.
Wagweno wana ngoma zao zinazoitwa mdumange ambazo huchezwa usiku kwa kutumia mianzi (mirangikwa kwa Kigweno) kama ile inayoitwa "nakuokera karughu vamaie kasembelele..." Sifa kuu ya Wagweno lugha yao haitumiki sana kwenye matambiko maana watambikaji wote hutumia lugha ya Kipare wanapokuwa katika mambo yao ya mila.
Kamusi fupi ya Kigweno kwenda Kiswahili
[hariri | hariri chanzo]
Kigweno |
Kiswahili |
ibata |
bata |
igonji |
kondoo |
kuchiikaa kwi? |
unakaa wapi? |
kuchilaghwa ii? |
unaitwa nani? |
kuchilaghwa iki ? |
unaitwa nani? |
kuelee mboa? |
umelala salama? |
kufumie kwi? |
unatoka wapi? |
kumwana wai? |
wewe ni mtoto wa nani? |
kundevukia mboa? |
umeamka salama? |
mboa kole iwe? |
salama sijui wewe? |
mburi |
mbuzi |
nguku |
kuku |
nguve |
nguruwe |
nguvo |
nguo |
njicha |
nzuri |
nthakame |
damu |
takwapfo? |
habari yako? |
thuruale |
tharawili |
asante kwa nguo mpya
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- lugha ya Kigweno kwenye Multitree
- makala za OLAC kuhusu Kigweno Ilihifadhiwa 22 Septemba 2015 kwenye Wayback Machine.
- lugha ya Kigweno katika Glottolog
- https://www.ethnologue.com/language/gwe
- https://www.african.gu.se/tanzania/weblinks.html Ilihifadhiwa 4 Oktoba 2006 kwenye Wayback Machine.
- https://www.linguistics.berkeley.edu/CBOLD/Docs/TLS.html (tovuti hiyo ina msamiati wa Kigweno)
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Maho, Jouni & Bonny Sands. 2002. The languages of Tanzania: a bibliography. (Orientalia et africana gothoburgensia, no 17.) Göteborg: Acta Universitatis Gothoburgensis. Pp ix, 428. ISBN 91-7346-454-6
Kitabu hiki kinataja marejeo mengine kama:
- Philippson, Gérard; Nurse, Derek. 2000. Gweno, a little known Bantu language of northern Tanzania. In: Lugha za Tanzania/Languages of Tanzania: studies dedicated to the memory of Prof. Clement Maganga (CNWS publications, no 89), uk. 231-284. Kuhaririwa na Kulikoyela K. Kahigi, Yared M. Kihore & Maarten Mous. Leiden: Research School of Asian, African and Amerindian Studies (CNWS), Leiden University.
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kigweno kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |