Benin
Jamhuri ya Benin | |
---|---|
République du Bénin (Kifaransa) | |
Kaulimbiu ya taifa: Fraternité, Justice, Travai (Kifaransa) "Udugu, Haki, Leba" | |
Wimbo wa taifa: L'Aube nouvelle (Kifaransa) "Mapambazuko mapya" | |
Mahali pa Benin katika Afrika ya Magharibi | |
Ramani ya Benin | |
Mji mkuu | Porto-Novo |
Mji mkubwa nchini | Cotonou |
Lugha rasmi | Kifaransa |
Idadi ya watu | |
• Kadirio la 2023 | 14 219 908[1] |
Benin, kirasmi Jamhuri ya Benin, ni nchi huru katika Afrika ya Magharibi. Awali iliitwa Dahomey.
Inapakana na Bahari ya Atlantiki upande wa Kusini, nchi ya Togo upande wa Magharibi, nchi ya Nigeria upande wa Mashariki na nchi za Burkina Faso na Niger upande wa Kaskazini.
Haihusiani na Mji wa Benin (Benin City) wala na Ufalme wa Benin wa karne ya 19.
Jiografia
[hariri | hariri chanzo]Nchi ya Benin iko kati ya Mto wa Niger upande wa Kaskazini na Bahari ya Atlantiki upande wa Kusini. Haina milima mirefu.
Idadi kubwa ya watu wanaishi katika tambarare za Kusini ambapo miji mikubwa ya Benin iko, ikiwa ni pamoja na mji mkuu, Porto Novo, na mji mkubwa zaidi, Cotonou. Sehemu za Kaskazini ni kavu hasa.
Nchi ya Benin inapata majira mawili ya mvua, Aprili-Julai na Septemba-Novemba. Pia kuanzia mwezi Desemba, kuna upepo ulioitwa harmattan, nao huleta vumbi na baridi wakati wa usiku.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Historia ya awali
[hariri | hariri chanzo]Ufalme wa Dahomey
[hariri | hariri chanzo]Ufalme wa Dahomey ulianzishwa katika nchi ya kisasa ya Benin.
Katika karne ya 17, ufalme huo uliotawaliwa na oba (ni cheo cha mfalme wake) ulienea sehemu kubwa ya Afrika ya Magharibi.
Dahomey ilianzishwa na Waaja baada ya uhamisho wao kutoka Togo kuja Benin ya leo. Jina la Dahomey linasemekana kuwa limetokana na neno la Kifon la "dan" lenye maana ya "nyoka" - dokezo la ibada ya nyoka kusini mwa nchi.
Jina la mfalme wa kwanza ni Do Aklin aliyekuwa mmoja wa wana watatu wa mfalme wa Ardra waliogawanya ufalme kati yao mnamo 1625 BK. Do Aklin aliunda mji wa Abomey ukawa mji mkuu wa Dahomey.
Waaja wa Abomey walichanganyikana na wenyeji wakawa kabila jipya la Wafon au Wadahomey. Waliratibu ufalme wao kwa kuupa serikali ya mfalme mwenye nguvu, wakaunda jeshi la kudumu.
Hasa mfalme Wegbadja aliweka utaratibu kwa vizazi vilivyofuata: mfalme alikuwa mtawala mkuu, mkoani au majimboni hapana watawala wa kieneo bali watumishi wake tu.
Ardhi yote ilitazamwa kuwa mali ya mfalme mwenyewe, mafundisho yaliyohakikisha malipo ya kodi kutoka kwa wakulima waliokubali ya kwamba nchi waliyoilima ni mali ya mfalme.
Mamlaka ya mfalme yalihakikisha nguvu ya Dahomey katika mazingira yake. Jeshi la kudumu lilimpatia chombo muhimu. Ndani ya jeshi hilo kulikuwa na kikosi kimoja cha pekee ambacho kilikuwa kikosi cha wanawake.
Wasafiri wa Ulaya walikiita kikosi hiki "Waamazoni" kutokana na askari wa kike katika masimulizi ya Wagiriki wa Kale.
Wegbadja na wafuasi wake walikaza pia umuhimu wa ibada za pamoja. Wafalme wenyewe na mizimu yao walipewa nafasi muhimu. Sadaka zilienda na kila nafasi, hasa sadaka kwa mizimu ya wafalme.
Dahomey na biashara ya watumwa
[hariri | hariri chanzo]Kulikuwa na utajiri mkubwa kwa sababu ya kufanya biashara na Wazungu, hasa Wareno na Waholanzi waliofika kuanzia mwisho wa karne ya 15.
Ufalme uliongezeka nguvu ya kiuchumi hasa kutokana na biashara ya watumwa. Kupaa kwa nguvu ya Dahomey kulikwenda sambamba na kuenea kwa wafanyabiashara Wazungu kwenye pwani za Afrika ya Magharibi walionunua watumwa kwa ajili ya safari ya Marekani, wakiuza silaha na bidhaa kutoka Ulaya.
Katika karne tatu za historia yake Dahomey ilikuwa kati ya wafanyabiashara wakuu wa watumwa. Pwani ya Benin ya leo ilijulikana kama Pwani ya Watumwa.
Jeshi la Dahomey lilikuwa na bunduki zilizonunuliwa kwa Wazungu wakiwauzia watumwa; silaha hizo zilitumika kwa ajili ya kupiga vita dhidi ya majirani na kujipatia wafungwa waliouzwa kama watumwa. Mapato kutoka biashara hiyo yaliwezesha wafalme wa Dahomey kununua silaha mpya.
Biashara ya watumwa iliendelea kwa karne tatu mpaka mwaka wa 1885.
Chini ya Wafaransa
[hariri | hariri chanzo]Kuanzia karne ya 18, ufalme wa Dahomey ulidhoofika mpaka Ufaransa uliweza kuuvamia mwaka wa 1892. Dahomey ikawa chini ya ukoloni wa Ufaransa kuanzia mwaka wa 1899 hadi ilipopata tena uhuru tarehe 1 Agosti 1960.
Baada ya uhuru
[hariri | hariri chanzo]Mpaka mwaka wa 1972 makundi mbalimbali walipigana vita, hatimaye Wakomunisti walianza kutawala chini ya kiongozi wao Mathieu Kérékou.
Hapo nchi ilipewa jina jipya, yaani Jamhuri ya Watu wa Benin, mwaka wa 1975 hadi 1991.
Tangu miaka ya 1980 nchi ilifuata mfumo wa soko huria. Kérékou alikuwa Rais hadi 1991, halafu tena miaka 1996-2006.
Katika uchaguzi wa Machi 2006, Yayi Boni alipata urais aliouanza tarehe 6 Aprili 2006.
Siasa
[hariri | hariri chanzo]Bunge la Benin lina viti 83. Huchaguliwa kila mwaka wa nne.
Rais ni mkuu wa serikali na wa nchi, naye huchaguliwa kila mwaka wa tano. Mgombea urais anatakiwa asiwe na umri wa miaka zaidi ya sabini.
Mikoa
[hariri | hariri chanzo]Kuna mikoa 12, nayo ni:
Watu
[hariri | hariri chanzo]Kuna makabila mbalimbali ambayo watu wake wanaongea lugha tofauti sana, k.m. Kihausa, lugha za Kisonghai, lugha za Kimande na lugha za Kifula.
Kabila kubwa kabisa ni lile la Wafon (39.2%).
Lugha rasmi ni Kifaransa.
Upande wa dini, Wakristo ni 42.8% (Wakatoliki 27.1%, halafu madhehebu mengi ya Uprotestanti). Waislamu ni 24.4%. Wafuasi wa dini asilia za Kiafrika 23.3% (hasa Vodun 17.3%). Asilimia 6.5 hawana dini yoyote.
Uchumi
[hariri | hariri chanzo]Uchumi wa Benin hauna nguvu sana, na hutegemea hasa kilimo, mazao ya pamba na biashara ndogondogo.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Orodha ya lugha za Benin
- Orodha ya nchi kufuatana na wakazi
- Orodha ya nchi za Afrika kulingana na idadi ya watu
- Orodha ya nchi za Afrika kulingana na msongamano wa watu
- Orodha ya nchi za Afrika kulingana na pato la taifa
- Demografia ya Afrika
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Adam, Kolawolé Sikirou and Michel Boko (1983), Le Bénin. SODIMAS, Cotonou and EDICEF, Paris.
Viungo ya nje
[hariri | hariri chanzo]- Tovuti rasmi ya Jamhuri ya Benin
- Ubalozi wa Benin nchini Marekano Ilihifadhiwa 14 Desemba 2005 kwenye Wayback Machine.
- allAfrica - Habari za Benin
- L'Araignée (Kifaransa)
- Allafrica news - Benin Ilihifadhiwa 3 Mei 2006 kwenye Wayback Machine.
- benininfo Bénin Info (Kifaransa)
- sonagnon.net Ilihifadhiwa 9 Mei 2006 kwenye Wayback Machine. (Kifaransa)
- Le Matinal
- LC2 international TV Ilihifadhiwa 27 Aprili 2006 kwenye Wayback Machine. (Live TV )
- La Tribune de la capitale Ilihifadhiwa 26 Mei 2020 kwenye Wayback Machine. (Kifaransa)
- Country Study: Benin
- CIA World Factbook - Benin Ilihifadhiwa 3 Mei 2006 kwenye Wayback Machine.
- MBendi - Information for Africa Ilihifadhiwa 24 Aprili 2006 kwenye Wayback Machine.
- US State Department - Benin
- Columbia University Libraries - Benin
- Open Directory Project - Benin Ilihifadhiwa 28 Aprili 2006 kwenye Wayback Machine.
- Stanford University - Afrika Kusini mwa Sahara: Benin
- Yahoo! - Benin Ilihifadhiwa 21 Agosti 2008 kwenye Wayback Machine.
- IT Consulting and certification Ilihifadhiwa 6 Januari 2007 kwenye Wayback Machine. (Kifaransa)
Nchi za Afrika | |
---|---|
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe | |
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika | |
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira |
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Benin kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
- ↑ "Benin". The World Factbook (kwa Kiingereza) (tol. la 2025). Shirika la Ujasusi la Marekani. Iliwekwa mnamo 23 Machi 2024.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) (Archived 2023 edition)