Athroskopia
Athroskopia (pia huitwa upasuaji wa kifundo) ni upasuaji wa kuingilia kwa kiasi kidogo kabisa ambapo uchunguzi na wakati mwingine matibabu ya uharibifu ndani wa kifundo hutekelezwa kwa kutumia athroskopu, aina ya hadubini inayoingizwa ndani ya kifundo kupitia mkato mdogo. Taratibu za kiathroscopia zinaweza kutekelezwa ama kutathmini au kutibu hali nyingi za mifupa pamoja na gegedu sogezi zilizoachana, gegedu za uso zilizoachana, ujenzi upya wa kano ya kushikilia goti mbele , na kusawazisha gegedu zilizoharibika.
Athroscopia kuliko upasuaji wazi wa jadi ni kwamba kifundo hakihitajiki kufunguliwa kikamilifu. Badala yake, kwa mfano athroscopia ya kifundo cha goti, mikato miwili midogo hufanywa - mmoja kwa ajili ya athroskopu na mmoja kwa ajili ya vyombo vya upasuaji vitakavyotumika katika pengo la goti na kuondoa funiko la goti kabisa. Hii hupunguza muda wa kupona na inaweza kuongeza kiwango cha mafanikio ya upasuaji kutokana na kiwewe cha chini kwenye tishu unganifu. Ni muhimu hasa kwa wanariadha wa kulipwa, ambao hujeruhi kifundo cha goti mara kwa mara na wanahitaji muda mfupi wa uponyaji. Kuna pia upungufu wa makovu, kwa sababu ya mikato midogo. Ugiligili wa kumwagiliwa hutumika kutanua kifundo na kutengeneza nafasi ya kupasulia. Wakati mwingine ugiligili huu huvuja hadi kwenye tishu laini zilizo karibu na kusababisha uvujaji na uvimbe wa giligili.
Vyombo vya upasuaji vinavyotumika ni vidogo kuliko vyombo vya jadi. Madaktari wapasuaji hutazama eneo la kifundo kwenye skrini ya video, na wanaweza kutambua au kurekebisha tishu za kifundo zilizoachana, kama vile kano na meniski au gegedu.
Inawezekana kitaalam kufanya uchunguzi wa kiathroscopia wa karibu kila kifundo katika mwili wa binadamu. Vifundo vinavyochunguzwa na kutibiwa kwa kutumia athroscopia aghalabu huwa ni vya goti, bega, kiwiko cha mkono, kifundo cha mkono, tindi la mguu, mguu, na nyonga.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Profesa Kenji Takagi wa Tokyo amesifiwa tangu jadi kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa kwanza wa athroskopia ya kifundo cha goti la mgonjwa mwaka wa 1919. Alitumia sistoskopu ya 7.3 mm kwa athroskopia zake za kwanza. Hivi karibuni imegunduliwa kuwa daktari wa Kideni Severin Nordentoft alitoa taarifa juu ya athroskopia za kifundo cha goti mwaka wa 1912 katika taarifa juu ya athroskopia ya goti ya pamoja mapema 1912 katika Kumbukumbu za Mkutano maalum wa 41 wa Shirika la Madaktari wapasuaji la Ujerumani huko Berlin. [1] Aliita utaratibu huo (kwa Kilatini) athroskopia genu. Nordentoft alitumia mchanganyiko wa chumvi tasa au wa asidi boriki kama chombo chake cha macho na aliingia ndani ya kifundo kwa kutumia pota kwenye mpaka wa nje wa kilegesambwa. Hata hivyo, si wazi ikiwa uchunguzi huu ulikuwa utafiti wa anatomia ya wagonjwa waliofariki au wanaoishi.
Kazi za kutagulia katika taaluma ya athroskopia zilianza miaka ya 1920 na kazi ya Eugen Bircher. [2] Bircher alichapisha majarida kadhaa katika miaka ya 1920 kuhusu matumizi yake ya athroskopia ya goti kwa madhumini ya kutambua ugonjwa. [2] Baada ya kutambua tishu zilizoachana kwa kutumia athroskopia, Bircher alitumia upasuaji wazi katika kuondoa au kurekebisha tishu zilizokuwa zimeharibika. Awali, alitumia thoracolaparoscopu ya Jacobaeus ya umeme kwa ajili ya taratibu zake za kutambua ugonjwa, ambayo ilionyesha mtazamo usio dhahiri wa kifundo. Baadaye, alifafanua mtazamo wa utofautishaji maradufu wa kuboresha hali ya kuonekana. [3] Bircher aliacha uhadubini mnamo mwaka wa 1930, na kazi yake ilitelekezwa sana kwa miongo kadhaa.
Wakati Bircher anakumbukwa mara kwa mara kama mvumbuzi wa athroskopia ya goti, [4] daktari mpasuaji wa Kijapani Masaki Watanabe, MD anapokea sifa kuu kwa kutumia athroskopia kwa upasuaji rekebishi. [5] [6] Watanabe alitiwa moyo na kazi na mafundisho ya Dr Richard O'Connor. Baadaye, Dr. Heshmat Shahriaree alianza kufanya majaribio ya njia za kukata vipande vya meniski. [7]
Athroskopu ya kwanza kutumika iliundwa kwa ushirikiano na watu hawa, na walifanya kazi pamoja kupiga picha wa kwanza wa rangi wa hali ya juu wa ndani ya kifundonisho[8] Taaluma ilinufaika sana kutokana na maendeleo ya teknolojia, hasa maendeleo katika nyuzi za optiki za kunyumbulika miaka ya 1970 na 1980.
Athroskopia ya goti
[hariri | hariri chanzo]Athroskopia ya goti imechukua nafasi ya athrotomi ya jadi katika mifano mingi. Siku hizi athroskopia ya goti inatekelezwa kwa kawaida kutibu jeraha la umbo la hilali, ujenzi upya wa kano ya kushikilia goti mbele na kwa kuvunjika maikro kwa gegedu. Athroskopia pia inaweza kutekelezwa kutambua ugonjwa na kukagua goti; hata hivyo, matumizi ya mwisho yamebadilishwa kwa kiasi kikubwa na upigaji picha wa kutumia mvumo wa sumaku.
Baada ya kufanya athroskopia ya goti utakuwa na uvimbe pande zote za kuzunguka goti, ni lazima uuruhusu uishe kabla ya kufanya mazoezi yoyote mazito au kutembea kwingi. Uvimbe anaweza kuchukua muda wowote kutoka siku 7-15 ili utulie kabisa. Ni muhimu kusubiri hadi uvimbe utakapoisha kwa sababu goti halitakuwa imara vilivyo kuweza kufanyiwa upasuaji, na linaweza kusababisha maumivu na wakati mwingine kufanya goti lifure zaidi.
Wakati wa athroskopia wastani ya goti, kamera ndogo ya nyuzi optiki (athroskopu) huingizwa ndani ya kifundo kupitia mkato mdogo wenye kadiri ya urefu wa milimita 4 (inchi 1/8). Ugiligili maalum hutumika kutazama sehemu za kifundo. Mikato zaidi inaweza kufanywa ili kuangalia sehemu zingine za goti. Kisha vyombo vingine vidogo hutumiwa na upasuaji unatekelezwa.
Upasuaji wa athroskopia wa goti hufanywa kwa sababu nyingi, lakini ipo shaka juu ya manufaa ya upasuaji kwa ajili ya kutibu ugonjwa wa baridi yabisi unaowaathiri wazee{/0. Utafiti maradufu unaodhibitiwa na kipozaungo pofu kuhusu upasuaji wa athroskopia kwa ajili ya ugonjwa wa baridi yabisi unaowaathiri wazee wa goti ulichapishwa kwenye Jarida la Udaktari la Uingereza Mpya (New England Journal of Medicine) mwaka wa 2002. [9] Katika utafiti huu wa vikundi vitatu, wakongwe 180 wa kijeshi wanaougua ugonjwa wa baridi yabisi unaowaathiri wazee waliteuliwa kuondolewa tishu zenye madhara wa athroskopia na uoshaji, au uoshaji wa athroskopia bila kuondolewa tishu zenye madhara (utaratibu tu wa kuiga kuondoa tishu zenye madhara kwa upasuaji, ambapo mikato ya juu juu kwa ngozi ilifanywa ili ionekane kwamba utaratibu wa kuondoa tishu zenye madhara ulikuwa umetekelezwa). Kwa miaka miwili baada ya upasuaji, wagonjwa walitoa taarifa kuhusu viwango vyao vya maumivu na walitathminiwa kwa mwendo wa kifundo. Si wagonjwa wala watathmini huru walijua mgonjwa yupi alipata upasuaji upi (hivyo nukuu ya "pofu maradufu"). Utafiti huo ulitoa taarifa, "Hakuna wakati ambapo mojawapo ya vikundi vya kuingilia viliripoti maumivu ya chini au uamilifu bora kuliko kundi la kipozaungo". [10] Kwa sababu hakuna faida iliyothibitishwa ya upasuaji huu kwenye mifano ya ugonjwa wa baridi yabisi unaowaathiri wazee wa goti, walipaji wengi husita kulipa madaktari wapasuaji na hospitali kwa kile kinachoweza kuchukuliwa kama utaratibu ambao unaonekana kusababisha hatari za upasuaji na faida isiyo hakika au isiyodhihirika. [11] Utafiti wa mwaka 2008 ulithibitisha kuwa hakuna faida ya muda mrefu kwa ajili ya maumivu sugu, zaidi ya dawa na tiba ya mwili. [12] Kwa kuwa moja ya sababu muhimu za athroskopia ni kurekebisha au kusawazisha umbo la hilali chungu na ilyoachana au kuharibika, utafiti wa hivi karibuni katika New England Journal of Medicine ambao unaonyesha kuwa kadiri ya 60% ya mitatuko hii haisababishi maumivu na hupatikana katika wagonjwa wasio na dalili zozote, unaweza kusaili zaidi urazini wa utaratibu huu. [13]
Athroskopia ya bega
[hariri | hariri chanzo]Athroskopia kwa kawaida hutumiwa kwa ajili ya matibabu ya magonjwa mbalimbali ya bega pamoja na kubanwa kwa misuli inayowezesha uzungushaji wa mkono kati ya mfupa wa mkono wa upande wa juu na upande wa chini wa skapula, akromioklavikula ya ugonjwa wa yabisi, mitatuko ya misuli inayowezesha uzungushaji wa mkono bega iliyoganda (kidonda fumbaza chenye kuganda), tendonitisi sugu na mitatuko nusu ya kano ndefu ya misuli ya mikono, vidonda vya SLAP na kuyumba kwa bega.
Athroskopia ya kiwiko
[hariri | hariri chanzo]Athroskopia ya kiwiko hutumika kuchunguza na kutibu dalili za jeraha sugu baada ya mkazo, uvunjikaji wa kiwiko na kano zilizoachana au kuharibika. Inaweza pia kutumika kuhakikisha uharibifu wa kifundo uliosababishwa na ugonjwa wa baridi yabisi.
Athroskopia ya uti wa mgongo
[hariri | hariri chanzo]Taratibu nyingi ingilizi za uti wa mgongo huhusisha kuondolewa kwa mfupa, misuli, na kano kupata na kutibu maeneo tatizi. Wakati mwingine, hali ya kifua (katikati ya uti wa mgongo) inahitaji daktari mpasuaji afikie eneo tatizi kwa kupitia ngome ya ubavu, na kurefusha muda wa kupona.
Taratibu za athroskopia (pia hadubini - ndani) za uti wa mgongo humruhusu daktari mpasuaji kufikia na kutibu aina mbalimbali za magonjwa ya uti wa mgongo na uharibifu wa chini zaidi kwa tishu zilizo karibu. Muda wa kupata nafuu unapunguzwa sana kutokana na kipimo kidogo cha m(i)kato kinachohitajika, na wagonjwa wengi hutibiwa bila kulazwa. [14] Viwango na muda wa kupata nafuu hutofautiana kulingana na ukali wa hali na afya ya mgonjwa kwa jumla.
Taratibu za athroskopia hutibu
- Mpenyezo wa diski ya uti wa mgongo na diski za kusawijika
- ulemavu wa uti wa mgongo
- uvimbe
- kiwewe jumla cha uti
Maelezo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Kieser CW, Jackson R W. Severin Nordentoft: The first arthroscopist. Athroskopia 2001, 17 (5) :532-5.
- ↑ 2.0 2.1 CH Bennett & C Chebli, ' Athroskopia ya Goti Ilihifadhiwa 30 Septemba 2007 kwenye Wayback Machine.'
- ↑ Kieser CW, Jackson RW (2003). "Eugen Bircher (1882-1956) the first knee surgeon to use diagnostic arthroscopy". Arthroscopy. 19 (7): 771–6. doi:10.1016/S0749-8063(03)00693-5. PMID 12966386.
- ↑ Böni T (1996). "[Knee problems from a medical history viewpoint]". Ther Umsch (kwa German). 53 (10): 716–23. PMID 8966679.
{{cite journal}}
: CS1 maint: unrecognized language (link) - ↑ Watanabe M: Historia ya upasuaji wa athroskopia. Katika Shahriaree H (toleo la kwanza): Kitabu cha kiada cha O'Connor cha upasuaji wa athroskopia. Philadelphia, JB Lippincott Co, 1983.
- ↑ Jackson RW (1987). "Memories of the early days of arthroscopy: 1965-1975. The formative years". Arthroscopy. 3 (1): 1–3. doi:10.1016/S0749-8063(87)80002-6. PMID 3551979.
- ↑ Metcalf RW (1985). "A decade of arthroscopic surgery: AANA. Presidential address". Arthroscopy. 1 (4): 221–5. doi:10.1016/S0749-8063(85)80087-6. PMID 3913437.
- ↑ Allen FR, Shahriaree H: Richard L. O'Connor-Shukrani. J Bone Joint 64A: 315, 1982.
- ↑ https://www.ncbi.nlm.nih.gov/entrez/query.fcgi?cmd=Retrieve&db=PubMed&list_uids=12110735 "Jaribio lililodhibitiwa la upasuaji wa ugonjwa wa baridi yabisi wa goti" N Engl J Med 2002 11 Julai, 347 (2) :81-8, Moseley JB, O'Malley K; Petersen NJ, Menke TJ, Brody BA; Kuykendall DH, Hollingsworth JC; Ashton CM; Wray NP
- ↑ "NEJM -- A Controlled Trial of Arthroscopic Surgery for Osteoarthritis of the Knee". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-02-18. Iliwekwa mnamo 2008-01-14.
- ↑ "Research diversity in DeBakey awards - From the Laboratories Online Newsletter at Baylor College of Medicine (January 2003)". Iliwekwa mnamo 2008-01-14.
- ↑ Kirkley A, Birmingham TB, Litchfield RB; na wenz. (2008). "A randomized trial of arthroscopic surgery for osteoarthritis of the knee". N. Engl. J. Med. 359 (11): 1097–107. doi:10.1056/NEJMoa0708333. PMID 18784099.
{{cite journal}}
: Explicit use of et al. in:|author=
(help); Unknown parameter|month=
ignored (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link) - ↑ Martin Englund, M.D., Ph.D., Ali Guermazi, M.D., Daniel Gale, M.D., David J. Hunter, M.B.,B.S., Ph.D., Piran Aliabadi, M.D., Margaret Clancy, M.P.H., and David T. Felson, M.D., M.P.H.; na wenz. (2008). "Incidental Meniscal Findings on Knee MRI in Middle-Aged and Elderly Persons". N. Engl. J. Med. 359 (11): 1108–1115. doi:10.1056/NEJMoa0708333. PMC 2897006. PMID 18784100. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-01-23. Iliwekwa mnamo 2010-10-18.
{{cite journal}}
: Explicit use of et al. in:|author=
(help); Unknown parameter|dead-url=
ignored (|url-status=
suggested) (help); Unknown parameter|month=
ignored (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link) - ↑ " Upasuaji wa uti kutumia hadubini-ndogo wenye ushambulizi mdogo . " 20 Juni 2005. Mchango wa Kliniki ya Cleveland kwa SpineUniverse.com
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Daktari mpasuaji wa athroskopia ya nyonga Ilihifadhiwa 9 Januari 2016 kwenye Wayback Machine. - Nigel Kiely (Daktari mpasuaji)
- Chama cha athroskopia cha Amerika ya Kaskazini Ilihifadhiwa 27 Septemba 2018 kwenye Wayback Machine.
- Athroskopia: Jarida la athroskopia na Upasuaji Unaohusiana
- Athroskopia ya kutambua ugonjwa - mafunzo ya Dr Angus Strover Ilihifadhiwa 21 Desemba 2009 kwenye Wayback Machine. - mtaalam wa GOTI
- Picha za mtatuko za SLAP ya bega Ilihifadhiwa 9 Septemba 2010 kwenye Wayback Machine.
- Maonyesho ya pande 3 ya goti Ilihifadhiwa 7 Desemba 2009 kwenye Wayback Machine.
- SpineUniverse Kituo cha taarifa kuhusu Upasuaji wa Uti wenye Uingiliaji Mdogo - Makala kutoka taasisi, mashirika, na wataalamu mbalimbali wa uti
- Makala kuhusu taratibu mbalimbali za athroskopia
- Udaktari wa tiba ya matatizo yasababishwayo na kushiriki katika michezo - athroskopia