Anime
Anime ni istilahi ya kutaja "Animation" au katuni hai kwa lugha ya Kijapani. Asili yake hasa ni Kiingereza, lakini katika baadhi ya sehemu, istilahi hii humaanisha "Japanese Animation", yaani, Katuni za Kijapani. Lakini nchini Japani, anime huwa wanalitumia pia kwa katuni yoyote ile bila kutazama maana halisi kwa lugha yao.
Baadhi ya katuni huchorwa kwa mkono, lakini vilevile zinaweza kutengenezwa kwa kutumia kompyuta. Kuna aina chungu nzima ya anime; unaweza kupata anime kuhusu michezo, mazingaombwe au mahaba. Hii ni baadhi ya mifano.
Anime huoneshwa katika televisheni, DVD na VHS, pia hutumiwa katika michezo ya video ya kompyuta.
Baadhi ya katuni za anime ni filamu, lakini zina wahusika wa hali za kikatuni na animation badala ya kuweka watu na maeneo ya kweli.
Anime hasa hutokana na kitabu cha katuni cha Kijapani kinachoitwa Manga na riwaya za picha. Wakati mwingine filamu za kawaida, yaani, filamu zinazohusisha mazingira ya kweli watu, mahali, na kadhalika huwa zinatokana na mifululizo ya anime.
Historia ya anime nchini Japani hutazamwa hasa kuanza kunako miaka ya 1900.