Andrea Kaggwa
Mandhari
Andrea Kaggwa (1856 hadi 26 Mei 1886, Munyonyo) ni mfiadini mmojawapo kati ya Wakristo 22 wa Kanisa Katoliki wanaojulikana na kuheshimiwa duniani kote kama Wafiadini wa Uganda.
Hao walikuwa wahudumu wa ikulu ya kabaka wa Buganda Mwanga II (1884 - 1903) ambao waliuawa kati ya tarehe 15 Novemba 1885 na tarehe 27 Januari 1887 kwa sababu ya kumwamini Yesu Kristo baada ya kuhubiriwa Injili na Wamisionari wa Afrika walioandaliwa na kardinali Charles Lavigerie.
Ndio wafiadini wa kwanza wa kusini kwa Sahara kuheshimiwa na Kanisa Katoliki kama watakatifu.
Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 3 Juni, lakini ya kwake mwenyewe tarehe 26 Mei[1].
Kabla ya kuuawa Andrea alikuwa mtu wa ukoo wa mfalme na kiongozi wa wanamuziki wake.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |